Katika muktadha wa mazungumzo ya haki ya tabianchi, sauti za wanawake zinaibuliwa kwa uwazi na haraka, zikihimiza Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Maattaiifa COP30 kuacha urithi wa kudumu kuhusu uhusiano kati ya jinsia na sera za tabianchi.

Wanaojadiliana wanashughulika na Mpango wa Hatua wa Belém kwa Usawa wa Kijinsia, unaotambua athari maalum za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake na kupendekeza hatua za kusaidia ufadhili wao, mafunzo, na kupata nafasi za uongozi.

Haki ya tabianchi na usawa wa kijinsia

Mpango huu, unaoshughulika na kipindi cha 2026-2034, unaweza kuimarisha mfumo wa msingi wa mbinu zinazojali jinsia katika mchakato wa mabadiliko ya haki, mikakati ya marekebisho na kupunguza athari, pamoja na mifumo ya fidia kwa hasara na uharibifu.

Ana Carolina Querino, Mwakilishi wa muda wa Shirika la Umoja wa Mataiifa la Maasuala ya Wanawake UN Women nchini Brazil, amesisitiza ujumbe ulioenea COP30 “Hakuna haki ya tabianchi bila usawa wa kijinsia.”

UN News pia imekusanya ushuhuda kutoka kwa wanawake wawili katika COP30 wanaofanya kazi kwa suluhisho thabiti za tabianchi. Hadithi zao zinaonesha umuhimu  na hitaji  la kuwekeza katika uongozi wa wanawake.

Nanci Darcolete mchaktaji wa taka kutoka São Paulo na mshauri wa taasisi ya Movimento de Pimpadores.

UN News/Felipe de Carvalho

Nanci Darcolete mchaktaji wa taka kutoka São Paulo na mshauri wa taasisi ya Movimento de Pimpadores.

Wachakataji wa taka

Nanci Darcolete, Mbrasil mwenye umri wa miaka 49, anayechakata taka, amefanya kazi kama mchakataji wa taka tangu 1999 katika mitaa ya São Paulo. Leo, anaongoza Pimp My Carroça, shirika linalolinda haki za wachakataji wa taka wafanyakazi wanaobadilisha vifaa vilivyotupwa kuwa rasilimali, hivyo kuzuia tani za taka kutupwa porini au kuchomwa katika mabaki.

Ameieleza UN News kwamba wachakataji wa taka wanachukua nafasi muhimu katika COP30, wakibainisha mchango wao katika kupunguza utoaji wa gesi zinazochangia joto duniani na kuhifadhi rasilimali za asili.

“Leo tunaona umuhimu wa wachakataji wa taka pia kushiriki katika kuunda mbolea kutoka katika taka za hewa ukaa. Hii itasaidia manispaa kuokoa pesa, kuhakikisha kipato kwa wachakataji na kuzuia tani za gesi ikichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vichafuzi vizito vinavyopatikana katika mazingira,” anasema Nanci Darcolete.

Wanawake wanaoongoza mnyororo wa uchakataji
Nchini Brazil, wanawake ndio wengi kati ya wachakataji wa taka na wanaongoza makundi mengi ya ushirika. Hata hivyo, wanaendelea kukumbwa na ubaguzi wa rangi na ukatili wa kijinsia mitaani. Wengi wanachanganya kazi hii na majukumu ya kifamilia, ikiwa ni pamoja na kutunza nyumba zao na kuwalea watoto na wajukuu wao.

Nanci anabainisha kuwa moja ya wasiwasi mkubwa wa wachakataji wa taka ni ongezeko la mawimbi ya joto na mafuriko kutokana na mabadiliko ya tabianchi hali zinazofanya kazi yao kuwa ngumu zaidi, hasa katika mtaa maskini.

Anaiomba COP30 itambue wanawake hawa kama “wadau wa mabadiliko”, kwa kuboresha miundombinu ya miji ili wapate kupunguza umbali wa kutembea, kupata maji, na kufaidika na mikataba ya malipo.

Kiongozi wa kesi za tabianchi

Kulia mwa bahari, Mariana Gomes, wakili wa kike wa Ureno mwenye umri wa miaka 24, amegundua katika sheria kile anachokiita “chombo muhimu zaidi” cha kupambana na janga la tabianchi na kusaidia jamii zilizo mstari wa mbele wa majanga. Yeye ni mwanzilishi na rais wa Último Recurso, shirika lililoanzisha kesi ya kwanza kabisa ya tabianchi nchini Ureno yenye kesi zaidi ya 170 zinazoshughulikiwa hadi sasa.

Mariana anaamini kuwa kesi za kisheria zinaweza kubadilisha maneno na ahadi za serikali kuwa hatua za lazima za tabianchi, hasa kufuatia tafsiri ya hivi karibuni ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, inayoziamuru nchi kuchukua hatua ili kupunguza ongezeko la joto duniani hadi chini ya nyuzijoto 1.5 °C.

“Ninaamini katika siku za usoni, tutaona kesi nyingi dhidi ya nchi hasa zile zinazohitaji kuongeza malengo yao, kutunga sheria za tabianchi na kulingana na malengo ya Mkataba wa Paris. Kwa kuwa leo hii zaidi ya hapo awali, tunabeba uzito wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki,” anasema.

Mwanasheria wa Kireno Mariana Gomes ni mjasiriamali na mwanaharakati wa mazingira

UN News/Felipe de Carvalho

Mwanasheria wa Kireno Mariana Gomes ni mjasiriamali na mwanaharakati wa mazingira

Haki ya mazingira yenye afya

Anasisitiza kuwa raia wanaweza kudai serikali zao kuhakikisha haki ya mazingira yenye afya na hali ya hewa thabiti. Nchini Ureno, anatetea maendeleo ya Mipango ya Hatua ya Tabianchi ya Manispaa nyaraka zinazobainisha jinsi mamlaka za mitaa zitakavyopunguza na kukabiliana na ukame, moto wa porini, mafuriko na majanga mengine.

Kwa Mariana, juhudi za kujenga mnepo na kupunguza madhara lazima zichukulie kuwa majanga ya tabianchi yanawaathiri wanawake kwa kiwango kikubwa, kuongeza hatari za ukatili wa kijinsia, kuhamishwa kwa nguvu, na mzigo mkubwa wa kulea.

Anaamini kuwa hatua za kisheria zinaweza kufanya zaidi ya kudai kupunguzwa kwa utoaji wa gesi au kuzuia miradi ya uchimbaji: zinaweza kufungua ufadhili na kusaidia fidia kwa jamii zilizokumbwa, zikisaidia kulinda haki za wanawake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *