[ad_1]

.

Chanzo cha picha, Maxence Melo

Muasisi wa JamiiForums, Maxence Melo, amesema jukwaa hilo linalazimika kukubali uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusitisha leseni yake ya maudhui kwa siku 90, japokuwa hawakubaliani nao.

“Tunalazimika kupokea uamuzi wa TCRA hata kama hatukubaliani nao. Tunatii mamlaka za nchi tunakotoa huduma. Hivyo, JamiiForums haipatikani kwa wateja wetu wa Tanzania,” Melo maarufu kama Max ameiambia BBC.

Amesema hata hivyo, utekelezaji wa sheria unapaswa kufuata taratibu zilizowekwa na Kanuni. “Kanuni zinataka aliyeathirika na maudhui kuripoti mwenyewe, mtoa huduma achukue hatua; kwetu haikuwa hivyo. Mlalamikaji ni Mamlaka, sio Rostam anayedaiwa kutosikilizwa. Bahati mbaya kuna wenzetu waliompa nafasi Rostam wakamnyima nafasi Polepole, hao hawajaguswa,” aliongeza.

TCRA ilitangaza kusitisha leseni ya maudhui ya JamiiForums na kuzuia upatikanaji wake nchini kwa madai ya kukiuka Kanuni za Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020 na marekebisho ya 2022. Mamlaka hiyo ilieleza kuwa JamiiForums ilichapisha taarifa “zisizo sahihi, za kukashifu na zenye lugha isiyofaa” dhidi ya Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *