Kadri dunia inavyoingia katika muongo muhimu wa jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu, ushirikiano kati ya Afrika na Ulaya umeendelea kuandika kurasa mpya za historia.

Miaka 25 ya uhusiano kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya umeimarisha ushirikiano wenye malengo ya pamoja, uwajibikaji wa pamoja, na utambuzi wa kina kwamba ustawi hudumu zaidi unapojengwa kwa pamoja.

Kuelekea kwenye Mkutano wa Saba wa AU–EU unaokutanisha viongozi mbalimbali nchini Angola, msisitizo umewekwa zaidi kwenye kutafuta suluhu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo na kwa pamoja.

Mwaka huu, mkutano huo unafanyika wakati sekta ya nishati duniani ikipitia mabadiliko ya kasi, na uwezo wa Afrika kuongoza mapinduzi ya nishati safi ukiwa dhahiri kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa rasilimali nyingi za nishati jadidifu zilizopo, idadi kubwa ya vijana, na masoko yanayokua, bara hili lipo mstari wa mbele katika enzi mpya ya ukuaji endelevu. Ulaya, kupitia mpango wa Global Gateway, inaingia kwenye uwekezaji wa muda mrefu na ushirikiano kama nguzo kuu ya mabadiliko haya.

Kwa pamoja, mabara haya mawili yanajiandaa kuzindua miradi mipya, kuimarisha biashara na ushirikiano, na kuharakisha uwekezaji katika nishati safi, uwekezaji utakaopeleka umeme majumbani na viwandani, na pia kuupa nguvu mustakabali wa pamoja uliojengwa juu ya uimara, fursa, na uaminifu.

Katika mahojiano maalum kuelekea kwenye mkutano huo, Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, anazungumza kwa uwazi na uthabiti kuhusu mwelekeo huo. Hii hapa ni sehemu ya mahojiano yake…

Swali: Ni matokeo gani yanayotarajiwa kutoka kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU)?

Jibu: Miaka 25 iliyopita, mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika jijini Cairo kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Viongozi walitoa ahadi thabiti kwamba amani na ustawi hudumu tu pale vinaposhikiliwa. Pale ambapo hatima zetu zinafungamana kwa kweli.

Dunia imebadilika tangu kufanyika kwa Mkutano wetu wa Cairo. Lakini uhusiano huu wa kipekee kati ya Ulaya na Afrika bado uko imara kama ilivyokuwa.

Huko Luanda, tutasherehekea ile mizizi tuliyoipanda katika mkutano wa pale Cairo. Na tutaupeleka ushirikiano huu wa kipekee kati ya Ulaya na Afrika katika ngazi ya juu zaidi.

Tutatangaza miradi mipya chini ya Global Gateway, mpango wa uwekezaji wa Ulaya kwa dunia iliyounganishwa zaidi. Tutafungua ukurasa mpya wa kibiashara na ushirikiano kati ya masoko yetu ya mabara haya mawili.

Na tutaongeza ushirikiano katika miradi ya nishati safi na malighafi muhimu, miradi inayoongeza thamani na ajira barani Afrika, kwa ajili ya watu wa Afrika. Na hivi ndivyo Ulaya inavyojenga ushirikiano; yaani ushirikiano wa kweli, endelevu.

Swali: Mnawezeshaje ujenzi wa kesho yenye nishati safi Tanzania?

Mwaka mmoja uliopita, Ulaya na Afrika Kusini walizindua kampeni ya ‘Scaling Up Renewables in Africa’, yenye lengo la kuhamasisha uwekezaji katika nishati safi; kusaidia kufikisha huduma ya umeme kwa watu milioni 600 ambao bado hawana huduma hiyo.

Na pia kuwavutia wawekezaji katika sekta hii inayokua kwa kasi barani Afrika. Wiki iliyopita, tulikusanya kiasi cha Euro bilioni 15.5 kwa ajili ya kufadhili miradi ya nishati safi kwa ajili ya kesho ya bara la Afrika na watu wake.

Kujenga uhusiano imara zaidi kati ya majirani ni sehemu muhimu ya usalama wa nishati. Kwa Tanzania, Umoja wa Ulaya unatekeleza miradi miwili ya Global Gateway, inayounganisha miundombinu ya nishati ya nchi hiyo na ile ya majirani zake wa nchi za Zambia, Kenya na Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *