Katibu katika Wizara ya ulinzi ya Marekani Dan Driscoll anakutana na ujumbe wa Urusi jijini Abu Dhabi kujadili mzozo wa Ukraine, vyombo vya habari vya Marekani vimethibitisha.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanafanyika zikiwa zimepita siku chache tangu ujumbe wa Marekani ukutane na wawakilishi wa Ukraine jijini Geneva katika juhudi zinazolenga kumaliza mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

Driscoll alikutana na ujumbe wa Urusi siku ya Jumatatu ya wiki, mazungumzo yao yakitarajiwa kuendelea hadi leo Jumanne kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Mazungumzo haya ya hivi karibuni yanafanyika baada ya mikutano kadhaa iliyofanyika nchini Switzerland kati ya Marekani na maofisa wa Ukraine, mikutano yenye lengo la kupata mwafaka wa mzozo unaoendelea.

Kulingana gazeti la The Financial Times, mkuu wa idara ya ujasusi ya Ukraine Kyrylo Budanov alitarajiwa kuhuduria mazungumzo hayo bila ya kutaja majina ya maofisa ambao wataiwakilisha Urusi.

Marekani imekuwa ikiishinikiza Ukraine kukubali mapendekezo ya yanayolenga kumaliza mzozo unaoendelea licha ya Kyiv kusema kwamba mapendekezo hayo yanaegemea kwa sehemu kubwa upande wa Urusi.

Kulingana na mapendekezo ya kwanza ya Marekani yenye vipengee 28, Ukraine itaachia baadhi ya maeneo yake kwa Urusi haswa Miji ya Donetsk na Lugansk mashariki ya nchi.

Ukraine imekataa mapendekezo hayo ikisema hayakubaliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *