#HABARI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Judith Kapinga, amewataka watumishi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kuboresha utendaji kazi na kuongeza ubunifu ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na uchumi wa kisasa.
Waziri Kapinga amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati wa juu, imara na inayojitegemea, hivyo taasisi za elimu ya juu zinapaswa kuchukua nafasi yao katika mabadiliko hayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya CBE, Prof. Zakaria Mganilwa, amempongeza Waziri Kapinga kwa mwongozo alioutoa na kusisitiza kuwa bodi itaendelea kusimamia mageuzi na maboresho ya chuo ili kiendane na matarajio ya Serikali na jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.