Siku hii ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake inadhimishwa kila mwaka 25 Novemba  na mwaka huu imebeda maudhui “Ukatili wa kidijitali ni ukatili halisi. Hakuna hoja yoyote kwa ukatili mtandaoni.”

Leo pia zinaanza siku 16 za uanaharakati kuelimisha umma kuhusu janga hii la ukatili na zitakamilika Desemba 10 Siku ya Haki za Binadamu Duniani. George Musubao kutoka Radio washirika wetu Kashindi iliyoko hukomjini Beni amezungumza na mmoja wa waathirika wa jinamizi hili la ukatili dhidi ya wanawake.

Vita ni kichocheo cha ukatili dhidi ya wanawake DRC

Katika majimbo nmengi, nchini DRC likiwemo jimbo la Kivu Kaskazini, vita na changamoto za makundi yenye silaha ndio chanzo cha ongezeko la kiwango kikubwa cha ukatili.

Bibi Kavira Malekera, ambaye jina lake lime badilishwa ili kumuhifadhi amekumbana na ukatili wa kingono baada ya kufungasha virago kukimbia vita nyumbani kwake Goma.

Akikumbuka safari yake Kavira anasema “Ninatoka katika jiji la Goma. Mimi ni mtu aliyekimbia vita. Mume wangu na watoto wangu wawili waliuawa huko Goma. Nilikuwa nimeumia sana, kwa hivyo nilikimbilia hapa Beni kama kila mtu mwingine. Nilitembea hadi Kanyabayonga na kisha hadi Kirumba. Nililala kwa siku mbili katika Mbuga ya wanyama ya Virunga. Watu huenda Beni, kwa hivyo mimi pia nilikuja hapa.”

Mambo yaliikuwaje alipowasili Beni?

“Nilipofika Beni na watoto wangu, tulikuwa tunaishi mitaani. Maisha yakawa magumu sana, kwa hivyo mama mmoja aliniambia nianze kumsindikiza kwenda mashambani, kwa sababu hapo ndipo ningeweza kupata chakula cha kuwasaidia watoto. Nilienda huko kulima na nikalipwa pesa 2,000 za Congo swa na Dola moja ya Marekani”

Safari yake ilikuwa ngumu , anaendelea kusema .”Yeye alibaki kwenye harusi. Shamba liko Mayangose. Nilipofika huko peke yangu, wanaume wawili walikuja na kuniuliza nichague kati ya kubakwa na kufa. Nilijibu kwamba singefanya chaguo, kwa hivyo walinifunga mikono na miguu, kisha wakanifunga macho. Nililia kama sijawahi kufanya hapo awali. Baada ya muda, walipasua nguo zangu zote na mwanaume wa kwanza akanibaka. Alipomaliza, mwingine akaja na kuendelea.”

Baada ya kudhulimiwa kingono uliwezaji kutoka shambani?

“Nilikuwa nimejivuta chini shambani, nikimwomba Mungu, nikimwambia kwamba unajua nilikuwa pale nikijaribu kuwasaidia watoto wangu kupata chakula. Baada ya safari ndefu, nilitoka karibu na kiwanda cha mafuta ya mawese, nikiwa uchi kabisa, kwa sababu nguo zangu zilikuwa tayari zimeungua”.

Lichaya aibu na fedheha aliyohisi hakusita kusala msaada na wasamaria walimsitiri

“Wanawake waliokuwa wanafanya kazi kwenye kiwanda hicho walinisaidia, nilipowaambia kilichonipata shambani. Kisha wakanileta hapa mjini.”

Hatimaye ulipofika mjini, mambo yalikuwaje?

“Mara tu nilipofika mjini, mwanamke aliyenipa shamba alinipeleka hospitalini. Huko, walinipa dawa ya Indocide kwa ajili ya kuzuia maambukizi. Hospitalini, nilikutana na akina mama wengine ambao pia walikuwa wamebakwa, kama mimi, karibu na Oicha. Madaktari walitupatia dawa, lakini tangu wakati huo, hakuna msaada zaidi hadi leo.”

Baada ya kitendo hiki kiovu, uhusiano wako na majirani ukoje?

“Hapa katika mtaa wangu, mimi hutumia siku zangu nyumbani. Ninapoenda kuchota maji kwa ajili ya watoto wangu, wanawake wengine hunidhihaki, wakisema, huyo ndiye aliyebakwa. Sina amani tena, mara tu ninapopita, baadhi ya watu hunicheka.”

Huyu ni kama tone tu la maji baharini kwani ukatili wa kingono DRC umekita mizizi kutokana na vita  na makundi ya wapiganaji wenye silaha .

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umekuwa msitari wa mbele kuwasaidia wanawake hawa waathirika kama Kavira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *