Mwezi mmoja baada ya kuchukuwa udhibti wa mji mkuu wa jimbo la Kaskazini mwa Darfur, wanajeshi wa Jenerali Hemedti bado wanajaribu kuficha mauaji wanayotuhumiwa kuyafanya katika mji huo, kulingana na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani. Watafiti hao, kwa ushahidi wa picha za setilaiti zilizopigwa mara kwa mara katika siku za hivi karibuni, wananyooshea kidole RSF kwa kuhusika na ukatili huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kama idadi ya vifo kutokana na kutekwa kwa mji wa El-Fasher na vikosi vya kijeshi vya Jenerali Hemedti haijulikani mwezi mmoja baadaye, ushuhuda kutoka kwa wakazi unaongezeka, ukiripoti mauaji ya halaiki, ubakaji, na mauaji ya kikatili yaliyofanywa wakati huo na Vikosi vay Msaada wa Haraka, RSF, ambavyo vinaendelea kuitupa miili hiyo hata leo ili kupoteza ushahidi.

Hilo, angalau, ndilo wanalodai watafiti kutoka Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani. Baada ya kuchanganua picha mbalimbali za setilaiti zilizopigwa katika siku za hivi karibuni, watafit hao wako tayari kwa lolote lile: kulingana nao, maumbo marefu, yenye urefu wa mita 1.5 hadi 2—wakiimaanisha miili—ambayo ilichomwa na kuzikwa.

Kwa mfano, picha hizi zikichukuliwa kila baada ya saa 12 hadi 24, zinaonyesha kwamba katika eneo la hospitali ya Saudi Arabia ambapo mauaji yalitokea, maumbo haya marefu huonekana mara kwa mara kabla ya kuchomwa moto na kisha kufunikwa na udongo, wanaelezea. Vitendo hivi pia vinaonekana huko Daraja Oula, kitongoji cha El-Fasher ambacho kilikuwa na idadi kubwa ya raia kabla tu ya shambulio la RSF, na ambapo walifanya mashambulizi ya nyumba kwa nyumba, wanaongeza watafiti hao.

Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu ya Yale pia yanabainisha kuwa, tangu jiji hilo litekwe, hakuna shughuli yoyote iliyorekodiwa katika masoko yake saba. Bado katika wilaya ya Daraja Oula, soko la Abu Qurun linaonekana kusitisha shughuli zake, ingawa watafiti wanabainisha uingiaji na utokaji wa magari ya kijeshi na, haswa, uwepo wa kontena, na kuwafanya wajiulize swali hili linalozua utata: wako wapi makumi ya maelfu ya wakazi wa El-Fasher ambao hawakuweza kutoroka mji huujiji, ambao bado hafikiki hadi leo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *