
“Naitwa Musisa Yusuph Onya, makazi wa hapa Hoima nataka kuzungumzia suala na tabia ya watu ambao wanapenda kuweka picha za udhalilishaji kwenye mtandao wa intaneti. Kwangu naona hilo si jambo zuri kama intaneti tunaitumia vibaya hivyo ni tabia mbaya sana kuweka picha za kuwadhalilisha wanawake kwenye intaneti”
Akaenda mbali zaidi na kusema kwa kufanya ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni
“Kwanza unakuwa umemdharau na kudhalilisha maisha yake, pili unakuwa umefanya kosa, hiyo ni kesi na tunataka kesi hiyo ihukumiwe na kuweka gerezani ili waweze kutambua kosa. Mfano wanaume wanaotumia vibaya intaneti kwa sababu utaona mtu mwweka picha yake nao wanaibadilisha wanawachojoa nguo na kuwacha utupu, hivyo unamuona mtu kama sio yeye nak ama unavyojua intaneti inakwenda kila mahali kila nchi na watu wenggi wanasoma na kuona unaharibu maisha yake na hiyo ni tabia mbaya sana ya kiwango cha juu.”
Mwisho ana wito
“Hivyo tunatoa wito kwa watu wote waahe tabia ya kutuma picha za utupu kwa wanaume , lakini serikali pia inatakiwa kuweka sheria kali kwa wadhalilishaji kuwakamata na kuwapeleka mahakamani, na wapelekwe gerezani. Hivyo wanaume wanapaswa kuishi pamoja na watu wengine vizuri kwenye dunia hii. Asante sana.
Shukran sana Mugisa kwa maoni yano.