Wataalamu waendelea kufanya matengenezo ya mizani MikeseWataalamu waendelea kufanya matengenezo ya mizani Mikese

MIKESE: TIMU ya maalumu ya wahandisi na wataalamu wa mizani imeanza kufanya matengenezo ya mifumo yote ikiwemo mfumo wa kupima magari yakiwa kwenye mwendo (Weigh in Motion) eneo la Mikese mkoani Morogoro.

Matengenezo hayo yanalenga kuhakikisha mizani inarejea kufanya kazi kwa ufasaha na viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa baada ya hapo awali kusabisha foleni katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Hatua hiyo inakuja baada ya Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kutoa maelekezo ya kurejeshwa kwa huduma hiyo haraka ambapo katika maelekezo hayo aliagiza kusimamishwa kazi watumishi waliohusika na uzembe huo wa mizani kutofanya kazi ili kupisha uchunguzi.

Wasimamizi hao ni pamoja na Meneja wa mizani kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Makao makuu, Mhandisi Leonard Mombia, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi John Mkumbo na Msimamizi wa mizani Mkoa wa Morogoro, Mhandisi British Mpeli.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na wizara hiyo, imewahakikishia wananchi kuwa wakati ukarabati ukiendelea, utaratibu maalumu umewekwa na unasimamiwa kwa weledi ili kuhakikisha magari yanaendelea kuhudumiwa kwa kufuata sheria za usafirishaji bila usumbufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *