
Papa Leo ameeleza kuwa dunia inayumba kutokana na tamaa na kuchagua mambo yanayodidimiza haki na amani. Ameyasema hayo akiwa ziarani Uturuki ambako amekutana na kuzungumza na Rais Recep Tayyip Erdogan.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani pia ameitolea wito Uturuki kulifurahia jukumu lake kama msuluhishi wa mataifa katika juhudi za kutafuta amani ya kudumu.
Erdogan ausifu msimamo wa Papa Leo juu ya Palestina
Kwa upande wake Rais Erdogan ameusifu msimamo wa Papa Leo kuhusu suala la Palestina baada ya mkutano wao. Erdogan amesema ana matumaini kuwa ziara hiyo ya kwanza ya Kimataifa ya Papa, itakuwa ya manufaa kwa utu wakati kukiwa na mivutano na hali ya mashaka ulimwenguni.