Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maswali mengi yameibuliwa kuhusu kuongezeka kwa matumizi ya bajeti iliyotolewa katika mfuko wa serikali ili kugharamia operesheni kadhaa za kijeshi tangu kuzuka kwa waasi wa AFC/M23 mashariki mwa nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na shutuma nyingi za ulaghai hasa kuhusu matumizi ya badgeti iliyotolewa ili kufadhili operesheni za kiusalama katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambapo ripoti za siri za uchunguzi uliofanyika hivi karibuni zimebaini matumizi mabaya ya pesa za serikali nchini humo.

Kati ya Mwaka wa 2021 na 2025, matumizi ya kipekee yanayohusiana na operesheni za usalama dhidi ya waasi wa AFC/M23 yaliongezeka nchini humo, zimebaini ripoti hizo;  Ingawa fedha zilizotengwa zilitumika kuongeza maradufu mishahara ya wanajeshi na kulipa wakufunzi wa kigeni, bali sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu matumizi ya baadhi ya fedha iliyotolewa.

Tangu kuanza tena kwa Uasi wa M23 mashariki mwa DRC—hasa zaidi tangu kuanguka kwa mji wa Bunagana mwezi Juni 2022, katika eneo la Rutshuru matumizi ya kipekee yanayohusiana na operesheni za usalama yameongezeka kutoka asilimia 51 tangu mwaka 2019.

Ripoti hizi pia zimeonyesha kuwa hakuna uwazi katika takwimu zilizotolewa na idara ya kitaifa ya usalama ambapo Kati ya 2021 hadi Juni 2025, kiwango cha matumizi ya pesa zilizotengwa kugharamia usalama wa taifa kilipanda hadi asilimia zaidi ya mia mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *