Rais wa Donald Trump amesema anapanga kuzuia raia kutoka nchi zinazoendelea kuingia nchini Marekani, siku moja baada ya raia wa Afghanistan kudaiwa kuwapiga risasi wanajeshi wawili jijini Washington.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Rais Donald Trump pia amesema serikali yake itachunguza upya vibali vilivyotolewa na serikali iliyotangulia kwa raia wa kigeni kuingia nchini humo.
Aidha, Trump aliongeza kuwa atakomesha manufaa na ruzuku zote kwa raia wasio wa Marekani, na pia kumfukuza raia yeyote wa kigeni ambaye ataonekana kuwa tishio la usalama.

Mamlaka pia zimetangaza kuwa zitapitia upya hadhi ya uhamiaji ya kila mkazi wa kudumu inayojulikana kama “Green Card” kutoka Afghanistan na nchi nyingine 18.
Siku ya Jumatano, Marekani ilisitisha kushughulikia maombi yote ya uhamiaji kutoka kwa raia wa Afghanistan, kwa sababu za usalama.