Duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu inatarajiwa kufanyika Agosti 2026, lakini kurejesha usalama kote Haiti ni muhimu kwa ajili ya uchaguzi, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Muda, chombo kilichotoa amri hiyo na kinachohusika na kuandaa uchaguzi. Mwenyejiti wa tume hiyo Jacques Desrosiers amenukuliwa akisema “Kurejesha usalama ni sharti la awali kwa kufanyika kwa duru ya kwanza” ya uchaguzi wa bunge na urais. Kwa muda mrefu haiti imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa na kiusalama, na hali imezidi kuwa mbaya tangu mapema mwaka 2024, wakati aliyekuwa waziri mkuu Ariel Henry alilazimishwa kujiuzulu na magenge yenye silaha ambayo bado yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu Port-au-Prince.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *