Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wametupiana lawama za kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano jana Jumanne, ikiwa ni siku mbili kabla ya Ikulu ya Marekani kuandaa hafla ya kusaini makubaliano ya kumaliza mapigano mashariki mwa nchi hiyo.