Tanzania: Gharama za Petroli zaendelea kushuka
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA), bei za mafuta ya petroli na ya taa, zimeendelea kushuka kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji kwa yale yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam.