Kocha wa Bayern Vincent Kompany alianzisha kikosi cha kwanza chenye wachezaji mahiri, akifahamu fika kuwa Berlin ndiyo timu iliyotilia kikomo msururu wao wa kushinda mechi katika Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga wiki chache zilizopita, walipowalazimisha sare ya mabao mawili.

Lakini katika mechi ya jana, Berlin walijifunga mabao mawili kisha bao la tatu la Bayern likatiwa kimyani na mshambuliaji wao Harry Kane.

Mabingwa wa kombe hilo la shirikisho VfB Stuttgart walipata ushindi wa 2-0 walipokuwa wakipambana na Bochum halafu Freiburg wakailaza Darmstadt 2-0 pia. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *