
Nawaf Salam ameyasema hayo licha ya hatua ya mazungumzo ya moja kwa moja yaliyofanywa kati ya nchi hizo mbili yakilenga kupunguza mivutano.
Matamshi ya Waziri Mkuu Salam yanakinzana na yale ya Waziri Mkuu wa Israel kwamba nchi yake itatuma mjumbe kwa mazungumzo na maafisa wa kidiplomasia na kiuchumi wa Lebanon.
Netanyahu alisema kuwa hiyo ni hatua ya awali ya kuunda msingi wa mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.
Lebanon na Israel wote walitangaza uteuzi wa wanachama wa kiraia katika kamati ambayo awali ilikuwa na wanajeshi watupu, ya kusimamia utekelezwaji wa usitishwaji wa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah uliosimamiwa na Marekani mwaka mmoja uliopita.
Wanachama hao wa kiraia wote walishiriki mazungumzo yaliyofanyika jana baina ya mataifa hayo mawili.