Macron vile vile atafanya mazungumzo kuhusu mahusiano ya kibiashara na XI. Rais Macron ambaye anaizuru China kwa mara ya nne tangu aingie madarakani mwaka 2017, anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Li Qiang kabla kusafiri kuelekea Chengdu.

China mara kwa mara hutoa matamko ya uwepo wa mazungumzo ya amani na kuheshimiana ila haijawahi kuilaani Urusi kwa uvamizi wake ilioufanya Ukraine mwaka 2022.

Serikali za Magharibi zinaituhumu Beijing kwa kuisaidia Urusina msaada muhimu wa kiuchumi katika vita na Ukraine, hasa kuipelekea silaha za kijeshi kwa ajili ya ulinzi wake.

Afisi ya rais wa Ufaransa imesema kuwa katika mkutano wao, Macron atamwambia Xi kuwa China inastahili kuacha kuisaidia Urusi kwa njia yoyote ile kuendeleza vita vyake nchini Ukraine.

Macron na Xi wakikagua gwaride la heshima
Macron na Xi wakikagua gwaride la heshimaPicha: Ludovic Marin/AFP

Ziara ya siku tatu ya Macron huko Beijing inafuatia mkutano wake na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, ambaye alitoa mwito kwa Ulaya kusimama na Kyiv wakati ambapo Rais Donald Trump wa Marekani anapambana na mpango wake wa kuvisitisha vita hivyo.

Mazungumzo ya kibiashara pia yamo kwenye ajenda

Macron pia anatarajiwa kujadili biashara na huyo mwenyeji wake, wakati ambapo Umoja wa Ulaya unakabiliwa na mapungufu makubwa ya dola milioni 357 kwa China.

“Ni muhimu kwa China kutumia zaidi na kuuza vichache nje ya nchi…na kwa wananchi wa Ulaya kuweka akiba ndogo na kuzalisha zaidi,” mshauri mmoja wa Macron alisema.

Macron atakuwa China hadi Ijumaa, ambapo hatua ya mwisho ya ziara yake itakuwa Chengdu katika mkoa wa kusini magharibi wa Sichuan.

Vyanzo: AFPE/Reuters

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *