Ripoti ya uchunguzi ya bunge la Kenya imewatuhumu wanajeshi wa Uingereza walioko nchini humo kwa unyanyasaji wa mara kwa mara wa kingono, mazoezi yasiyo salama na ukiukaji wa mazingira. Ripoti hiyo imebainisha kuwa mienenendo hiyo mewafanya wanajeshi hao ajinabi kujiona kama “kikosi vamizi”.

Ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii na Kamati ya Ulinzi na Mahusiano ya Nje ya Bunge la Kenya imeakisi hasira na malalamiko mkabala wa vitendo vinavyofanywa na Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la Uingereza nchini Kenya (BATUK), ambacho hupokea maelfu ya wanajeshi wa Uingereza kila mwaka.

Wizara ya Ulinzi ya uingereza imealiambia shirika la habari la Reuters kwamba “inajutia sana” matatizo yaliyoripotiwa kufuatia na uwepo kijeshi wa nchi hiyo huko Kenya na kwamba  iko tayari kuchunguza madai yoyote mapya mara ushahidi utakapowasilishwa.

Kesi maarufu zaidi inahusu mauaji ya  Agnes Wanjiru mwenye umri wa miaka 21 yaliyojiri mwaka 2012  karibu na kambi ya mafunzo ya Waingereza huko Nanyuki. Mshukiwa mkuu, mwanajeshi wa Uingereza kwa jina la Robert Purkiss, alikamatwa nchini Uingereza mwezi uliopita baada ya kampeni ya miaka kadhaa ya familia ya Wanjiru na wanaharakati wa Kenya.

Mwanajeshi huyo wa Uingereza amekanusha kuhusika na mauaji ya Wanjiru. Ripoti ya kamati ya Ulinzi na Mahusiano ya Nje ya Bunge la Kenya imeeleza kuwa, vikao vya wanajamii vilivyoendeshwa karibu na uwanja wa mafunzo vimefichua “visa vya kutatanisha” ya ubakaji, kushambuliwa, watoto waliotelekezwa na majeraha ya kazi ambayo yanawaathiri Wakenya waliokodishwa ili kuondoa silaha ambazo hazijalipuka bila ya kuwa na vitendea kazi kwa ajili ya usalama wao. 

Katika ripoti hiyo, wabunge wa Kenya pia wamewasilisha ushahidi wa utupaji taka zenye sumu na uharibifu mwingine wa mazingira.

Kwa upande wake Kitengo cha Mafunzo cha Jeshi la uingereza nchini  Kenya (BATUK) kimeiambia kamati  ya Ulinzi na Mahusiano ya Nje ya Bunge la Kenya kwamba sera yake haivumilii kabisa unyanyasaji wa kingono na kinasisitiza kuwa, ukaguzi wake wa mazingira unadhiirisha namna unavyotii pakubwa sheria za Kenya.

Makubaliano ya sasa ya ulinzi kati ya Kenya na Uingereza yalitiwa saini mwaka wa 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *