
Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la watu walemavu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kulingana na taarifa kutoka mashirika ya kiutu, ongezeko hili linahusishwa na vita vinavyodumu mara kwa mara ambavyo vimeathiri maisha ya maelfu ya raia eneo hilo la mashariki mwa DRC
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Anifa SAFARI alijeruhiwa kwa risasi miaka miwili iliyopita katika maadamano yakiraia mjini Goma yaliopelekea mamia ya watu kujeruhiwa nawengine kubaki walemavu.
Nakumbuka wakati tulishambuliwa mimi pia nilipigwa risasi mguuni na mama mzazi akapigwa risasi nakufariki,ndio mana naomba haki kufanyika ili sisi mayatima tupewe haki yetu
Ongezeko hilo la watu walemavu limekuwa ni tatizo kubwa la kibinadamu kutokana na changamoto zinazo wakabili watu hao, Herman Chirimwami anatoka shirika la ukingo wa walemavu, PAPH mjini Goma.
Hapo awali walemavu walikua niasilimia 15 lakini kwa sasa hesabu imeongezeka katika mkoa wa kivu kaskazini
Kauli yake inatiwa mkazo na Mungu Akonkwa safari, kukutoka asasi zakiraia mkoani kivu kaskazini.
Tuliuanza mwaka huu na watu wasio walemavu lakini kwa sasa wengi wamepoteza miguu na mikono,na yote hayo nikutokana na vita kwa hiyo tunawataka wote kuacha
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mkoa wa Kivu Kaskazini umekuwa ukitikiswa na machafuko ya vita, jambo ambalo limesababisha watu zaidi ya 23000 kupoteza makazi yao limesema shirika lakuwahudumia wakimbizi duniani UNHCR huku watu wanaoishi na ulemavu wakiendelea kupitia changamoto ambazo viongozi wa AFC/M23 wameahidi kumaliza.