
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Hamas Jumatano ilikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya wapiganaji wake kutoka kwenye handaki huko Khan Younis na kuwashambulia wanajeshi wa Israel kwenye eneo ambalo wanalidhibiti.
Israel iliishutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano ya amani, kabla ya kufanya mashambulizi ya anga ya awali. Hata hivyo, Hamas imetoa taarifa inayolaani vikali mashambulizi hayo ya Israel huko Khan Younis.
Mwili wa mateka mwingine watambuliwa
Wakati huo huo, mabaki ya mwili yaliyokabidhiwa na Hamas kwa Israel yamegundulika kuwa ya mateka raia wa Thailand.
Jeshi la Israel limesema Alhamisi kuwa Sudthisak Rinthalak alitekwa kutoka Israel wakati wa mashambulizi ya Hamas na makundi mengine ya wanamgambo Oktoba 7, mwaka 2023.
Mwili wake umekuwa ukishikiliwa na kundi la Islamic Jihad katika Ukanda wa Gaza. Alifariki Mei 16, 2024 akiwa na umri wa miaka 42.