Akichezacheza sokwe wengine, Carter anashindwa kuficha uchangamfu wake, anapokuwepo ndani na hifadhi ya milima ya Mahale, iliyopo mkoani Kigoma.

Akiwa na umri wa miaka 40, Carter ni mtoto kwa sokwe jike maarufu kwa jina la Calliope, aliyefariki mwaka 2009 akiwa na miaka 51.

Carter alikuwa na ndugu zaje wawili, wa  kiume mmoja; aitwaye Cadmas, ambaye alikufa mwaka 2010 akiwa na miaka 18 baada ya kushambuliwa na aliyekuwa kiongozi wa kundi wakati huo (Alpha Male) aitwaye Pimu, na ndugu yake jike, Carmen.

“Kwa sasa, umri wake mkubwa unamfanya sokwe Carter kuonekana kama babu mlezi, mtulivu, mwema, mwenye kupenda kukaa karibu zaidi na sokwe wadogo kuliko madume wenye nguvu wanaoongoza kundi lake la Sokwe wa Mahale,” anasema Philipo Hassan, askari uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Muda mwingi, Carter huonekana akitembea kwa utulivu ndani ya kundi kubwa la sokwe, akifurahia maisha ya amani anayoyaishi na jamii ya kundi lake.

Na nyakati zingine hupendelea kupata utulivu wa kujitenga na vurugu ambazo husababishwa na madume wa kundi lake.

“Pia hupenda kukaa na watoto, kuwatazama, na kucheza nao huku akitengeneza uhusiano wa kipekee unaowafanya watoto kumpenda na kumfuata kila mara,” anaeleza Philipo kutoka TANAPA.

Ikolojia inaonesha kuwa, madume wengi wa Sokwe, wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30 huepuka sana kucheza na sokwe wadogo, wakihofia ‘kupotezewa heshima’ na ‘watoto hao’, katika jamii ya koo zao.

Uongozi katika ukoo wake

Ingawa ni dume aliyewahi kufika nafasi ya tano katika uongozi wa ukoo wake, Carter hajawahi kufika uongozi wa juu. Tangu akiwa kijana, Carter hajawahi vurugu za aina yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *