Rais wa Marekani Donald Trump, pamoja na marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda, Félix Tshisekedi na Paul Kagame, wamesaini makubaliano ya amani huko Washington siku ya Alhamisi, Desemba 4, 2025, huku mapigano makali yakiendelea kurindima katika maeneo mbalimbali. Rais wa Marekani amezungumzia “muujiza mkubwa,” huku marais wa Kongo na Rwanda wakichukua tahadhari zaidi. Hawakupeana mikono.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vincent Souriau, mwandishi wa RFI nchini Marekani, ambaye alikuwepo Washington, ameelezea kwamba viongozi hao wawili wa Afrika walifika “saa mbili” kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, muda mfupi kabla ya saa 8:00 mchana kwa saa za huko (saa 3:00 usiku saa za Afrika ya Kati). Na walifika katika mji mkuu wa Marekani kwa saa “tofauti” kwa sherehe ya sehemu mbili: karamu iliyoandaliwa na Donald Trump “katika faragha” katika Ikulu ya White House, ikifuatiwa na sherehe ya utiaji saini mbele ya kamera na waandishi wa habari katika Taasisi ya Amani ya Marekani, “shirika linalofadhiliwa na Bunge la Marekani ambalo lilibadilishwa jina jana (Jumatano) kuwa ‘Taasisi ya Amani ya Donald Trump’ kwa kutarajia sherehe hii.”

Wakati wa kutia saini makubaliano haya ya amani, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, alionya kwamba kutakuwa na “heri na hasara” katika utekelezaji wa “mikataba hii ya Washington.”

“Ni jukumu letu barani Afrika kufanya kazi na washirika wetu ili kuimarisha na kupanua amani hii”, alisema Paul Kagame, Rais wa Rwanda.

Mwenzake kutoka DRC, Félix Tshisekedi, alisifu “mwanzo wa njia mpya” ambayo itakuwa “yenye kulazimishwa” na “ngumu sana.”

“Mkono wetu umenyooshwa kwa ushirikiano wa amani unaotegemea kuheshimiana, kutoingilia kati, na mapigano ya pamoja dhidi ya makundi yenye silaha”, alisema Félix Tshisekedi, Rais wa DRC.

“Huu utakuwa muujiza mkubwa,” alisema Donald Trump, akisifu makubaliano “yenye nguvu na ya kina”.

Donald Trump ameahidi kwamba “kila mtu atapata pesa nyingi.”

Bilionea huyo wa Marekani “alifichua kwamba wakuu hao wawili wa nchi walikuwa na majadiliano mengi nyuma ya pazia katika Ofisi ya Oval,” Vincent Souriau anaripoti. Félix Tshisekedi na Paul Kagame wanajulikana kwa kutofautiana, lakini Donald Trump aliwaita “wanaume jasiri.” Pia aliwasalimia wakuu wa nchi na wawakilishi wa Togo, Uganda, Qatar, Falme za Kiarabu, na wengine, ambao walialikwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Viongozi hao wawili wa Kiafrika, katika siku zijazo, “watatumia muda mwingi kukumbatiana na kushikana mikono,” Donald Trump alitabiri kwa msisitizo wake wa kawaida, ingawa rais wa Rwanda wala wa Kongo hawakujaribu kutoa ishara yoyote huko Washington: hata baada ya kusainiwa kwa makubaliano, hawakutazamana au kupeana mikono. Hali hii haikumzuia rais wa Marekani kuendelea kwa kudai kwamba “kila mtu atapata pesa nyingi” kutokana na “mikataba hii ya Washington,” ambayo ina mwelekeo wa kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *