Marekani. Jina lake halisi ni Aliaune Damala Badara Akon Thiam, maarufu kama Akon, ni moja ya mastaa wakubwa wa muziki wa R&B na Hip-Hop duniani ambaye ngoma zake zilivuka mipaka ya kimataifa.

Akon alizaliwa Novemba 16, 1973 huko St. Louis, Missouri, Marekani, lakini alikulia Senegal ambako ndiko iliko asili yake.

Sauti yake ya kipekee, midundo yenye mvuto, na uwezo wa kugusa hisia za wasikilizaji wa kila kona ya dunia, yalimfanya kuwa msanii wa kiwango cha kimataifa.

SAFARI YAKE

Akon alianza tasnia ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000. Nyimbo zake kama ‘Locked Up’ zilimfanya aonekane kama msanii mwenye sauti halisi ya kusimamia hisia za watu.

Ngoma hiyo iligusa hisia za watu waliokuwa wanakabiliana na changamoto za jamii, ikiwamo masuala ya hofu, uhuru, na maisha magumu. Nyimbo hiyo iliunganisha mashabiki wengi.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Baada ya mafanikio ya ‘Locked Up’, Akon aliachia nyimbo kama ‘Lonely’ na ‘Smack That’, ambazo zilimpa umaarufu wake si tu Marekani bali Ulaya na dunia nzima.

Nyimbo hizo ziliunganisha mchanganyiko wa R&B na Hip-Hop, pamoja na midundo ya Afrobeat, jambo lililovutia mashabiki wa tamaduni tofauti. Ushirikiano wake na mastaa wengine wa kimataifa kama Snoop Dogg, Eminem, Pitbull na Lady Gaga, ulisaidia kueneza sauti yake na kuibua hisia tofauti kwa mashabiki wa muziki wa Ulaya.

Hivi karibuni amejikita kwenye miradi ya nishati mbadala, maendeleo ya Afrika, na kusaidia jamii.

Kwenye tuzo za Grammy alichaguliwa mara tano kwenye vipengele tofauti ingawa hakuchukua tuzo yoyote tangu aanze muziki.

Kati ya kazi zake zilizowahi kuingia Grammy ni Smack That aliomshirikisha Eminem, ‘I Wanna Love You’ na Snoop Dogg, ‘Bartender’ na T‑Pain, na albamu yake ya ‘Konvicted’.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Tuzo alizowahi kuchukua ni Billboard Music Awards. Akon alipata tuzo kadhaa za Billboard, ikiwamo kwenye kipengele cha “Top Hot 100 Artist” na “Top R&B/Hip-Hop Artist” kupitia albamu kama Konvicted na Freedom.

Hii inatambulisha umaarufu wake barani Marekani na Ulaya, kwani Billboard inakadiria mafanikio kulingana na mauzo, uchezwaji wa radioni na mtandao.

Nyingine ni MTV Europe Music Awards (EMA) amewahi kutambuliwa na EMA kwenye vipengele viwili “Best R&B” na “Best Male Artist.

Akon amepewa heshima na kutajwa kuwania BET Awards, ikiwemo kwa ‘Best Male R&B Artist’ na “Viewer’s Choice Award.”

BET ni moja ya chaneli kubwa ya Marekani inayolenga wasanii weusi, na tuzo hizi zinamthibitisha kama kiongozi wa muziki wa R&B wa kizazi chake.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MAISHA BINAFSI

Akon aliwahi kufichua kwenye kipindi cha redio cha Angie Martinez mwaka 2006 kwamba yeye ni anaamini katika maisha ya mwanaume kuwa na wake wengi na anao uwezo wa kuwahudumia kadri anavyotaka. Kwa mujibu wa mwimbaji huyo, wanaume kwa asili ni waenezaji kizazi na anaamini utamaduni wa kuwa na wake wengi ungepunguza kiwango cha ukatili wa majumbani nchini Marekani.

Akon aliripotiwa kuliambia jarida la Blender mwaka 2017 kwamba ana watoto watano (wavulana wanne na msichana mmoja) kutoka kwa wanawake 3 tofauti. Tangu wakati huo, mwimbaji huyo amepunguza sana kuzungumzia taarifa za maisha yake binafsi kwenye vyombo vya habari.

Orodha ya wake waliowahi kutajwa kuwa ni wa Akon, ingawa kwa sababu mbalimbali wengine waliripotiwa kujiondoa: Yupo Tomeka Thiam (ambaye alimuoa mwaka 1996, ambaye amefungua kesi ya kuomba talaka Septemba 11, 2025), Tricia Ana, Rachel Ritfield (anatajwa kujitoa katika uhusiano wake na staa huyo), yupo pia

Rozina Negusei na mwanamke mwingine ambaye hakutajwa hadharani.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Kufikia Desemba 2022, Akon alitajwa kuwa na watoto tisa.

Mwaka 2023, mwanamke mmoja alidai hadharani kuwa yeye ni mmoja wa wake wanne wa Akon, na kwamba wake hao wanne wako Atlanta, L.A., na Afrika.

Akon ni Mwislamu na pia amedai kuwa hanywi pombe kabisa.

Staa huyu aliwahi kumiliki mgodi wa almasi nchini Afrika Kusini na alikanusha kuwepo kwa almasi za vita (blood diamonds) katika mahojiano ya mwaka 2007, akisema: “Siamini katika almasi za vita. Hiyo ni filamu tu. Fikiria. Hakuna aliyewahi kufikiria au kujali kuhusu almasi za vita hadi filamu Blood Diamond ilipotoka.”

Hata hivyo, baadaye alikubali kuwepo kwa almasi za vita na akasema alikuwa mmiliki mwenza wa mgodi barani Afrika ambao ulikuwa umejikita kuepuka kutumia almasi za vita na kutoa sehemu ya faida kusaidia jamii za eneo husika. Mwaka 2020, alifichua kuwa aliondoka kwenye biashara hiyo kutokana na athari zake mbaya za kimaadili, akidai kuwa “ni mbaya kuliko biashara ya dawa za kulevya.”

Akon alisema katika kipindi cha ITV2 The Hot Desk kwamba yeye ni shabiki wa klabu ya Ligi Kuu ya England, Chelsea.

ALBAMU ZAKE

Trouble (2004)

Konvicted (2006)

Freedom (2008)

El Negreeto (2019)

Akonda (2019)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *