Miongoni mwa walionufaika na mpango huu wa kuwawezesha watoto wenye ulemavu ni Kibra, mwanafunzi wa darasa la saba ambaye ndoto zake za kupata elimu zilikuwa zikizongwa na changamoto za ulemavu alioupata akiwa bado mtoto mchanga.
“Ulemavu huu ulinitpata nikiwa mtoto wa umri wa miezi miwili. Nilipotaka kutoka nje, ilinibidi nishikilie kitu kwa msaada. Ilikuwa ngumu kwangu kutembea umbali mrefu, hivyo marafiki zangu walinisaidia kwenda na kurudi kutoka shuleni.”
Licha ya hali hiyo, nia ya Kibra ya kuendelea na masomo haikuyumbishwa. Walimu wake waliitambua dhamira yake, na hapo safari yake mpya ikaanza. Anaeleleza..
“Walimu wangu walielewa shauku yangu katika elimu na kunisajili kwenye mpango huu, kisha nikaunganishwakwa Mikal mtaalamu wangu wa kijamii.”
Kibra, Mwanafunzi wa darasa la saba ambaye ndoto zake za kupata elimu zilikuwa zikizongwa na changamoto za ulemavu alioupata akiwa bado mtoto mchanga amepata fursa ya kushiriki elimu jumuishi.
Kupitia mpango huu, Kibra amepata msaada wa kifedha, vifaa vya shule, pamoja na kiti mwendo unaosaidia kurejesha matumaini yake na kumwezesha kuendelea na safari yake ya elimu bila vikwazo vya awali.
Leo, akiwa na tabasamu na matumaini mapya, Kibra anaangalia mbele kwa ndoto iliyojaa matumaini na uthabiti.
“Nina ndoto ya kuishi kwa kujitegemea siku moja, bila kutegemea wengine. Kwa watu wengine kama mimi, nataka kuwasaidia kwa kuwaambia kwamba, kuwa na nguvu, fanya kazi kwa bidii, soma na ujifunze. Pia nataka kutoa ujumbe huu, usikate tamaa na uwe mwenye nguvu.”
Kwa msaada huo wa OCHA na CERF, hadithi kama ya Kibra zinaendelea kuandikwa upya zikitoa nuru katika jamii ambazo zimeathiriwa na changamoto, na kulea kizazi kipya chenye matumaini, nguvu na uwezo wa kutimiza ndoto zao.