Msemaji wa ofisi ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa Seif Magango akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari akiwa Nairobi amesema tangu katikati ya Novemba, watu kadhaa wakiwemo wasomi, maafisa wa asasi za kiraia na viongozi wa kisiasa wamekamatwa.

Baadhi wanadaiwa kukamatwa na watu wasiojulikana na ambao walikuwa na silaha. Kufikia sasa, ikiwa ni wiki tano baada ya matukio ya vurugu, mamlaka za Tanzania bado hazijatoa taarifa kuhusu idadi ya waliouawa, mazingira ya vifo hivyo wala ripoti za watu waliotoweka. “Mnamo Desemba 3, polisi ilitangaza marufuku ya jumla kwenye maandamano ya nchi nzima ya Siku Kuu ya uhuru. Tunatoa wito kwa serikali kuondoa hatua hii inayopitiliza. Tunaiomba serikali kuviagiza vikosi vya usalama kupanga na kufanya shughuli zao kwa njia ambayo itawaruhusu Watanzania kutekeleza kikamilifu haki zao za msingi.”

Serikali ya Tanzania imeanzisha uchunguzi kuhusu machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu na kusababisha vifo vya watu wengi na uharibifu wa mali, ambao upinzani na waangalizi wa kigeni walidai haukuwa wa haki na usawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *