Mapigano yachacha Congo saa chache baada ya hafla ya kusaini makubaliano ya amani ya Trump
Kundi la waasi la AFC/M23 linaloungwa mkono na Rwanda, ambalo liliteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Congo mwaka huu na halifungwi na makubaliano ya Washington, limesema vikosi vinavyoitii serikali vinaendesha mashambulizi mengi.