Duniani kuna zaidi ya aina 800 ya ng’ombe wa maziwa. Lakini si kila ngombe hutoa maziwa katika kiwango kinachohitajika. Kuna ng’ombe ambao hutoa maziwa kiwango kidogo na wengine kiwango kingi kutegemea na aina zao.
Zifuatazo ni aina 7 za ng’ombe wenye maziwa mengi duniani;
1. Aina ya Ng’ombe wa Holstein

Source: Getty Images
Huyu ni ng’ombe wa Fresian ambaye hutoa maziwa kwa kiwango kikubwa mno. Kila mwaka yeye huzalisha maziwa lita 32,740 kumaanisha ni . Asili yake ni uholanzi. Fresian wanapatikana pia katika nchi ya Ujerumani.
2. Aina ya Ng’ombe mwekundu wa Norway

Ng’ombe mwekundu wa Norway ni maarufu sana kwa ajili ya maziwa ambayo anazalisha yenye ubora wa hali ya juu. Aina ya huyu ng’ombe inapatikana kule Norway na huhitaji malezi na kutunzwa kwa makini ya hali ya juu ili azalishe maziwa mengi. Yeye huzalisha maziwa lita 10,000 kila mwaka kumaanisha ni lita 27 kwa siku.
N’gombe huyu aligunduliwa kule Norway mwaka wa 1935.
3. Aina ya Ng’ombe wa Kostroma

Source: Getty Images
Huyu anapatikana kule Urusi, ambapo aligundulika karne ya 20. Ng’ombe aina ya Kostroma sawa na Ng’ombe mwekundu wa Norway. Ng’ombe huyu huzalisha maziwa lita 10,000 kila mwaka kumaanisha ni lita 27 kila siku. Huishi kwa miaka 25 tu na huhitaji lishe bora ili kuzalisha maziwa mengi.
4. Ng’ombe aina Kahawia wa Uswizi

Ng’ombe wa Kahawia wa Uswizi ni maarufu sana kwa kutoa maziwa ya kutengeneza jibini ,yani cheese. Yeye huzalisha lita 9,000 za maziwa kila mwaka kumaansha ni lita 24 kila siku. Yeye ni mnyama mwenye asili ya Uswizi.
5. Aina ya Ng’ombe mwekundu wa Kiswidi

Source: Getty Images
Ng’ombe huyu ni maarufu sana kwa kuwa yeye huishi maisha marefu na yenye afya. Ana urefu wa sentimita 140. Yeye huzalisha maziwa lita 8,000 kila mwaka ambapo ni lita 21 kila siku, kisha ana uzito wa kilogramu 600. Yeye hupatikana kule Uswidi.
6. Ayrshire

Source: Getty Images
Ayrshire ni maarufu kwa kuwa huwa na fya nzuri na mwili wake una kinga ya kukabili magojwa mbalimbali. Vilevile ni rahisi sana kumtunza. Ng’ombe huyu huzalisha maziwa lita 7,831 kila mwaka ambapo ni lita 21 kila siku, kisha ana uzito wa kilogramu 600. Ayrshire hupatakina Skotland na Uholanzi.

Pia soma
Hazina ya Riadha: Mamilioni Ambayo Omanyala Ametia Mfukoni Kutoka Diamond League Mwaka wa 2026
7. Angeln

Source: Getty Images
Angeln ni ng’ombe maarufu kwani maziwa yake huwa na chembechembe za mafuta mengi. Yeye huzalisha maziwa lita 7, 570 kila mwaka. Ng’ombe aina ya Angeln anapatikana Ujerumani.
Mwandishi ni Kevin Anindo, Kaunti ya Nairobi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
