Majina ya mataifa yalitajwa moja baada ya jingine katika droo ambayo iliamua kuwa Argentina na nyota wake Lionel Messi itaanza safari ya kutetea taji lao dhidi ya Algeria na Marekani itafungua dimba dhidi ya Paraguay.
Miezi 27 baada ya safari ya kufuzu kuanza, timu kutoka mabingwa mara tano Brazil kwa wageni wapya Cape Verde, Curacao, Jordan na Uzbekistan walibaini wapinzani wao wa hatua ya makundi katika kinyang’anyiro hicho kilichotanuliwa hadi mataifa 48 na mechi 104 ambacho kitaanza Juni 11 nchini Marekani, Canada na Mexico.
Hafla ya kupanga makundi katika Ukumbi wa sanaa wa Kennedy mjini Washington ilianza kwa Rais wa Marekani Donald Trump kutokea tuzo mpya ya amani iliyotolewa na FIFA, shirikisho la soka ulimwenguni.
Mabingwa mara tatu Argentina watafungua dimba Juni 16 dhidi ya Algeria kabla ya kucheza dhidi ya Austria na Jordan katika Kundi J.
Marekani, ambayo ilitinga nusu fainali ya Kombe la Dunia la kwanza 1930 na robo fainali 2002, inaanza Kundi D dhidi ya Paraguay mnamo Juni 12. Kisha watacheza dhidi ya Australia na kumaliza na ama Uturuki, Romania, Slovakia au Kosovo Juni 25.
Wenyeji wenza Mexico watafungua dimba Mjini Mexico Juni 11 dhidi ya Afrika Kusini katika Kundi A, ikiwa ni marudio ya sare ya 1 – 1 ya mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2010 mjini Johannesburg. Kisha watakutana na Korea Kusini n kufunga hatua ya makundi na ama Jamhuri ya Czech, Ireland, Denmark au North Macedonia.
Mechi zote kuanzia robo fainali zitachezwa kwenye ardhi ya Marekani, kabla ya fainali ya Julai 19 mjini East Rutherford jimboni New Jersey.
England, iliyoshinda taji lake la pekee mwaka wa 1966, itacheza dhidi ya Croatia, Ghana na Panama katika Kundi L.
Brazil itafungua dimba dhidi ya Morocco waliofika nusu fainali 2022, kisha waangushane na Haiti na Scotland katika Kundi C.
Uhispania inaorodheshwa nafasi ya juu kabisa duniani, bingwa wa 2010, itacheza dhidi ya Cape Verde, Saudi Arabia na Uruguay katika Kundi H, wakati Ujerumani baada ya kucheza na Curacao, itacheza dhidi ya Ivory Coast na Eqauador katika Kundi E.
Mabingwa mara mbili Ufaransa wataanza Juni 15 dhidi ya Senegal. Les Bleus walipoteza 1 – 0 dhidi ya Simba wa Teranga katika mechi ya ufunguzi mwaka wa 2002, mjini Seoul, Korea Kusini. Ufaransa kisha itakabiliana na Iraq au Suriname katika Kundi I na kufunga kazi ya makundi dhidi ya Norway. Mechi itawakutanina washambuliaji hatari Kylian Mbappe na Erling Haaland.
Ureno yake Cristiano Ronaldo, kama tu Messi anayetarajiwa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya sita, ana Kundi K dhidi ya Uzbekistan, Colombia na Congo, Jamaica au New Caledonia. Ikiwa Ureno watashinda Kundi lao, Ronaldo na Messi huenda wakakutana katika robo fainali.
Makundi mengine ni Pamoja na:
G: Belgium, Egypt, Iran, New Zealand.
B: Canada, Switzerland, Qatar na Italy, Bosnia-Herzegovina, Wales au
Northern Ireland.
F: Netherlands, Japan, Tunisia na Sweden, Ukraine, Albania na Poland.
Hakuna timu iliyowahi kupata ubingwa mara mbili mfululizo tangu Brazil iliposhinda 1958 na ’62, na ni mataifa nane pekee yaliyowahi kubeba taji hilo kubwa kabisa la kandanda. Italy imeshinda mara nne na Uruguay mbili.
Dpa