
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo watu wengine 14 walijeruhiwa na kupelekwa hospitali wakiwa na majeraha ya risasi. Shambulio hilo lilitokea leo mapema katika baa isiyo na leseni katika kitongoji cha Saulsville, magharibi mwa Pretoria.Wakati polisi ikiendelea kuwatafuta washukiwa, imetaja umri wa watoto waliouawa kuwa ni mvulana mwenye umri wa miaka 3, mwingine wa 12 na msichana wa miaka 16. Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa yenye viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani na ilirekodi mauaji zaidi ya 26,000 mwaka 2024 ikiwa ni wastani wa zaidi ya mauaji 70 kwa siku.