
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, leo hii ametoa wito wa kuharakisha kupelekwa kwa kikosi cha kimataifa cha kufuatiliaWaziri huo ametoa onyo hilo akisema wanahitaji kukipeleka haraka iwezekanavyo kikosi hicho kwa sababu upande mmoja, ambao ni Israel, kila siku unakiuka usitishaji wa mapigano, kwa hiyo wanahitaji waangalizi. Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Misri aliongeza kuwa kivuko cha Rafah kwa upande wa Misri kuelekea Gaza “hakitakuwa lango la kuwahamisha watu. Ni kwa ajili ya kupeleka misaada ya kibinadamu na huduma za matibabu tu.”