Kiongozi huyo wa Ujerumani ataanzia ziara yake mjini Amman, ambako amepangwa kukutana na Mfalme Abdullah II wa Jordan. Baadaye leo hii atapokelewa na Rais wa Israel Isaac Herzog mjini Jerusalem. Ingawa mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu yamepangwa kufanyika kesho Jumapili.Merz pia atatembelea Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Wayahudi (Yad Vashem) ili kuweka shada la maua, jambo ambalo ni desturi ya kila ziara ya kwanza ya kansela wa Ujerumani nchini Israel.Ziara hiyo inatarajiwa kujikita katika kurekebisha uhusiano uliokuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha zaidi usitishaji wa mapigano huko Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *