Dar es Salaam. Mlimani City, najiburuza kilofalofa kwenye zile ‘tailizi’ zao. Shingo na macho ndo viungo vinavyoteseka kwa wakati huo. Gen Z wa kike na kiume na nguo zao za Ghounzhou wanameremeta ka’ taa za Xmass.

Masimu mapana mapana, macho matatu. Wamejirembo wao kama wao na simu zao wamezivisha mpaka midoli. Wamejaza vitu vitu mwilini kama duka la Mangi wa Kibosho.

Kuna ‘taim’ utadhani upo Ethiopia, Madagascar au Shelisheli. Gen Z wa Bongo kuwatambua kiasili ni ngumu. Zamani mtu akitembea tu unajua kabisa huyu Muha, tena wa Kazulamimba. 

Kila kabila ukiachana na lugha na utamkaji wa maneno. Yalikuwa na viashiria fulani vya asili au vya majanga. Mikono iliyoathiriwa na ukoma, miguu na funza, meno na maji au kwashakooo. 

Ukiachana ndui ambalo lilikuwa jambo la kawaida. Kuna kabila zenye tattoo za asili, mfano kwa Wamakonde au Wagogo. Imejini lipo kabila lazima mwanya uwepo kwa meno ya chini. Usibishe.

Mtoto wa Dar ungemtambua kwa uongeaji wake. Mnyakyusa ama Muhaya maumbo yao ilitosha bila kusubiri ‘aksenti’ yao. Kuna wale wenye makomwe au viguu vyao vilitosha kujua asili yake. U feel me?

Zamani ukiona pisi ina magaga miguuni. Yaani nyayo zimepasuka pasuka, unajua kabisa hii ni ‘medi ini Tentemeke Sanga’ Makete ‘oni ze wani endi tuu’. Watu tulijuana namna hii. 

Unakuta pisi nyeupeee ina shepu ila miguu ya mbu. Unajua toleo hili ‘streiti fromu kwa gaizi gaizi gaizi’. Au pisi inaongea bila kituo, unajua hii inatoka kule milimani kwa kina Januari. 

Ndo maana utasikia wewe mbishi Muha. Unaongea kama Mzaramo au Msambaa. Ama mfupi kama Mluguru au umezubaa sana kama Msukuma. Uungwana tuliona ni kama kuzubaa. 

Kimsingi tulitambuana kwa alama nyingi sana. Watu pekee ambao bado wanadumisha mila, ukiacha Wamasai, basi ni Wachaga. Hawa jamaa walishashindwa kutemana na ile ‘aksenti’ yao. 

Sasa hawa Gen Z ni vigumu sana kujua asili zao. Wamevurugika na kujimiksi sana, ni rahisi kujua kalelewa na ‘singo maza’ kuliko asili yake. Ni kibaya zaidi wengine ni ngumu kujua hata jinsi yake.

Gen Z wanajuana kwa Instagram, Tiktok, X kama siyo Telegram. Kule ndiko iliko dunia yao, kule ndiko viliko vijiwe vyao. Wakati tunakua wengi tulishinda kwenye viwanja vya soka. 

Hawa Gen Z wanashinda kwenye maduka ya kamari. Na kuangalia soka badala ya kulicheza. Wakati siye tulienda disko toto hawa wa sasa wanaenda gesti toto. Noma.

Wakati milenia tulikuwa mbele ya muda, Gen Z wako mbele ya umri. Wakati zamani watu wa mikoani walivutiwa na ‘aksenti’ ya Dar. Leo hii hata kiswahili hawakijui watu wa Dar.

Ukitaka kujua hawajui, muwekee simu kwa kiswahili. Badala ya send iwe tuma, pasiwedi andika nywila. Hata ATM kwa kiswahili wengi huvurugwa. Ni kizazi flan feki feki. 

Kuna tofauti ndogo sana ya Gen Z na Milenia. Sisi Milenia tulitumia akili na harakati, lakini hao Gen Z hutumia mizuka na taharuki. Ni kizazi kisichotafakari kabisa na wanataka leo siyo kesho. 

Pisi za Milenia, ziliharibiwe ule usichana wao kwa baiskeli ama michezo. Pisi za Gen Z zinaanza kazi kazi bima kupitia ‘fildi’. Simu ndo muongozo wao kwa kila kitu.

Kuna mishangazi zamani tuliita mishangingi. Mishangazi ya leo mitaa yao ni Mbweni, Ununio, Masaki, Mbezi na maeneo flan classic. Kuwakuta huku uswazi ni ngumu na yanalea sana vimarioo vya mjini.

Mashangingi ya enzi zetu yalijaa kwenye taarabu. Lango la Jiji, Max Bar Ilala, balaa ni Njenje pale Gogo Hotel Moroko. Wachache sana waliolea vitoto vya kiume, ila kubeba waume za watu ulikuwa mchezo wao.

Ukisikia mume yupo Magomeni, ujue kuna shangingi limemficha. Mashangazi vinywaji vyao ni bia zinazokuja na meli. Mashangingi ulevi wao ilikuwa kula kungu ili macho yalegee kama nyaya za simu za mezani.

Mishangazi mikononi wana simu za gharama. Shingoni ni cheni na vidani vya gharama, wengi wao wana elimu kubwa. Wana ndinga flan hivi na hukaa bar za kishua.
Hawapayuki wala kucheka ovyo. 

Mashingingi yalijua kujishebedua. Mikononi hina, miguuni vikuku vya shanga na gauni za kung’aa. Ukizingua, linakuzingua zaidi kwa kukusuta na masingi. Linakujazia watu dakika moja, noma kwako.
Mishangazi ndo mishangingi.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *