
Nchini Benin, kufuatia tangazo la jeshi kwamba “ameondolewa madarakani,” Rais Patrice Talon amehutubia taifa Jumapili, Desemba 7, 2025, kwenye televisheni ya kitaifa. Amesema kwamba
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“kitendo hiki cha usaliti hakitabaki hivo bila kuadhibiwa” na kwamba “hali imedhibitiwa.” Asubuhi hiyo mapema, waasi walielekea nyumbani kwake na ikulu ya rais. Milio ya risasi ilisikika, na wanajeshi kadhaa walikamatwa, kulingana na vyanzo vya usalama. ECOWAS ilitangaza kupeleka wanajeshi kutoka Kikosi chake baada ya jaribio hili la mapinduzi.
Rais wa Benin Patrice Talon alionekana kwenye televisheni ya kitaifa siku ya Jumapili jioni, Desemba 7, kutangaza jaribio la mapinduzi kwamba limezuiwa. “Ningependa kuwahakikishia kwamba hali imedhibitiwa kabisa na kwa hivyo kuwaalika kuendelea na shughuli zenu kwa utulivu jioni hii,” alisema. “Usaliti huu hautabaki bila kuadhibiwa,” aliongeza.
“Nchi yetu leo imepitia matukio makubwa sana,” alieleza Rais Talon, akishutumu “kundi dogo la wanajeshi” ambao, “kwa kisingizio cha madai ya uwongo, wameanzisha uasi kwa lengo la kushambulia taasisi za Jamhuri na kuyumbisha usalama wa taifa letu, na hivyo kudhoofisha utaratibu wa kidemokrasia.”
“Wajibu wa Jamhuri unanilazimisha, kwa nafasi yangu kama Rais wa Jamhuri, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi, na mdhamini wa utulivu usalama wa nchi, kuchukua hatua zinazofaa kuzuia mipango ya wahuni hawa wanaotaka kuturudisha kwenye historia ya kumbukumbu mbaya. (…) Kwa hivyo, kwa kushirikiana na uongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama, nimeanzisha hatua muhimu za kudumisha amani na kuhakikisha usalama wa wote,” Mkuu wa Nchi aliongeza.
“Nchi yetu imepitia matukio makubwa sana leo”, Rais wa Benin Patrice Talon alizungumza kwenye televisheni ya kitaifa.