Dar es Salaam. Katika kuhakikisha wateja wananufaika na huduma zitolewazo na wateja wake ikiwemo kampeni, Benki ya Absa Tanzania imewazawadia wateja wake Sh21 milioni katika droo ya kampeni ya ujanja ni kuswipe na kadi ya Absa.

Absa Bank Tanzania imetangaza washindi wa droo ya pili wa kampeni yake inayoendelea ya Ujanja ni Kuswipe na kadi ya Absa.

Jumla ya Sh18 milioni zimekabidhiwa kwa washindi watatu wa kila mwezi, pamoja na Sh3 milioni zilizogawiwa kwa washindi wa wiki ya nane.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Ndabu Swere, Mkurugenzi wa Benki ya Wateja Binafsi, amesema: “Tumeridhishwa na jinsi kampeni ya Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa ilivyowagusa wateja wetu.”

“Inatia moyo kuona wengi wakihamasika matumizi ya miamala ya kidijitali na kadi, ambayo si tu ni rahisi kutumia bali pia yanaongeza ujumuishwaji wa kifedha na usalama. Tunawashukuru sana wateja wetu kwa uaminifu wao na ushiriki wao.”

Katika hafla hiyo, washindi watatu wa kila mwezi waliotangazwa ni Dk Fauz Twalib aliyelamba Sh10 milioni, Xuan Liu Sh5 milioni, na Joseph Mafuru Sh3 milioni.

Vilevile, washindi sita wa kila wiki wa wiki ya nane kila mmoja akiibuka na zawadi ya Sh500,000, amba ni: Anita Mselle, Michael Marshall Pemba, Idris Aziz Almamad Mazar, Shamma Kurban Hussein Dhirani, Christel Ulomi, na Gheorghe Alexandru.

Samuel Mkuyu, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Kidijitali wa benki hiyo, ameongeza kwa kusema dhamira yao ni  kuwezesha Afrika ya kesho, pamoja hatua moja baada ya nyingine.

Katika hatua nyingine, Felician Hechei, mshindi wa safari ya kifahari kwenda kwenye tamasha maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini.

Amesema, “Safari ilikuwa ya kipekee kabisa. Kuanzia usafiri wa daraja la biashara, hadi huduma za kifahari katika hoteli ya nyota tano, Absa walijali kila kitu. Tamasha lenyewe la Champagne lilikuwa tukio la kipekee maishani, na nawashauri wote washiriki kampeni zijazo za Absa.”

Kampeni ya Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa inaendelea hadi mwisho wa Desemba 2025, na itafikia kilele kwa droo kubwa ya Januari 2026 ambapo mteja mmoja atajinyakulia Sh30 milioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *