Daktari huyo mwandamizi kutoka hospitali kubwa jijini Dar es Salaam, aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotambulishwa amesema waliagizwa kutosema chochote na simu zao zilichukuliwa na kuchunguzwa kama zilikuwa na picha ama video yoyote.

Amesema wakati akiwa kwenye zamu Novemba Mosi, zaidi ya wagonjwa wake 200 walichukuliwa na watu ambaohawakuwa wamevalia sare yoyote, waliofika hospitalini na malori ya rangi ya kijani inayofanana na rangi ya jeshi.

Ameongeza kuwa walichukua miili iliyokuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, kilichokuwa kimefurika, hadi miili mingine kulazwa chini na kulingana na mfanyakazi mmoja wa chumba hicho, zaidi ya miili 300 ilichukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *