
Taarifa zinaeleza kuwa mamia ya wanajeshi wa Burundi na Kongo wamelazimika kukimbilia nchini Burundi. Wizara ya mambo ya nje ya Burundi imelaani kile ilichokiita uchokozi wa Rwanda, kwa kudai kuwa Kigali ilifanya mashambulizi ya makombora Jumatatu usiku karibu na mkoa wa Cibitoke na kuwajeruhi watu wawili, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 12.
Vurugu zimeongezeka eneo hilo ikiwa ni siku chache tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani kati ya Rwanda na DRC yaliyosimamiwa na Marekani, huku rais wa Kongo Felix Tshisekedi akimtuhumu mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kwa kukiuka makubaliano hayo.