
Netanyahu anatarajiwa kukutana na Trump huko Florida huku serikali ya Marekani ikijaribu pia kumshawishi Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sissi kuhudhuria mazungumzo hayo.
Taarifa hii imetolewa baada ya Netanyahu kusema kuwa awamu ya pili ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza itaendelea mara tu Hamas itakapokamilisha zoezi la kurejesha mabaki ya mateka wa mwisho.