
Kenya imetuma kikosi kipya cha maafisa wa polisi 230 nchini Haiti siku ya Jumatatu ili kuimarisha ujumbe wa kimataifa ambao tayari umeombwa na mataifa mengi kusiriki, na ambao umeshindwa kudhibiti magenge yenye nguvu ya silaha nchini humo. Kutumwa kwa kikosi hiki kunakuja huku Haiti ikiendelea kuwa katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na usalama, huku sehemu kubwa ya mji mkuu ikiwa chini ya udhibiti wa magenge yenye silaha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kenya imetuma mamia ya maafisa wa polisi wengine ili kuchukuwa nafasi ya vikosi vilivyomaliza misheni yao nchini Haiti siku ya Jumatatu, kwa lengo la kudumisha shinikizo kwa magenge nchini Haiti huku mgogoro wa kisiasa na usalama ukiendelea.
Magenge ya wahalifu yamekuwa yanaedelea kuzorotesha usalama nchini Haiti kwa muda mrefu, na kusababisha machafuko na ukosefu wa utulivu ambao umezidi kuwa mbaya tangu mwanzoni mwa mwaka 2024, walipomlazimisha Waziri Mkuu wa wakati huo Ariel Henry kujiuzulu.
Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba makundi yenye silaha sasa yanadhibiti 90% ya mji mkuu, Port-au-Prince, ambapo mauaji, ubakaji, uporaji, na utekaji nyara ni hutokea mara kwa mara huku kukiwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa.
Ili kuwasaidia polisi wa Haiti waliozidiwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kupelekwa kwa ujumbe wa usalama wa kimataifa nchini Haiti mwaka 2023, ukiongozwa na Kenya.
Hata hivyo, timu hii isiyo na vifaa na ufadhili wa kutosha—ikiwa na takriban maafisa wasiopungua 1,000 tu kati ya 2,500 wanaotakiwa—iko mbali na kukidhi ukubwa wa changamoto hiyo.
Siku ya Jumatatu, maafisa wa polisi 230 wa Kenya waliwasili Haiti, huku wengine wapatao 100 wakiondoka nchini, chanzo cha serikali ya Haiti kimeliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.
Mwishoni mwa mwezi Septemba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kuundwa kwa kikosi kikubwa cha kupambana na magenge nchini Haiti.
Haiti ambayo ni nchi maskini zaidi barani Amerika, haijafanya uchaguzi kwa miaka tisa na kwa sasa inaongozwa na serikali ya mpito.
Uchaguzi wa wabunge na urais umepangwa kufanyika majira ya joto ya mwaka 2026.