Burundi imelaani “tabia ya kivita” ya Rwanda siku ya Jumatatu, Desemba 8, ikiishutumu nchi hiyo kwa “kurusha mabomu” katika ardhi yake, na kuwajeruhi watu wawili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi, tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Cibitoke, ambayo inapakana na Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni “mtoto wa umri wa miaka 12,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi imesema, ikilaani “uchochezi wa Rwanda.”

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rwanda ilishtumu wanajeshi wa Burundi kwa kurusha mabomu katika ardhi yake, katika mji wa Bugarama, unapopakana na Kamanyola upande wa DRC na Rugombo upande wa Burundi. 

Wanajeshi wa Burundi, wanasaidia wanajeshi wa DRC, FARDC, wanaoungwa mkono na Wazalendo katika vita dhidi ya waasi wa M23, ambao wamechukuwa udhibiti wa miji kadhaa na maeneo mengi, katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, mashariki mwa DRC.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanaendelea kusonga mbele katika uwanja wa mapambano huko mashariki mwa Kongo na kukaribia kuchukua udhibiti wa mji wa Uvira unaopakana na nchi jirani ya Burundi, baada ya kuchukuwa hivi karibuni udhibiti wa maeneo ya Katogota, Luvungi, Lubarika na Luberizi, katika uwanda wa Rusizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *