Kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindwa nchini Benin, mkutano usio kuwa wa kawaida wa baraza la mawaziri umefanyika siku ya Jumatatu, Desemba 8, katika ikulu ya rais, ukiongozwa na Rais Patrice Talon. Uongozi wa juu wa kijeshi na polisi ulishiriki katika kikao hiki. Siku ya Jumapili, rais aliahidi kuhakikisha usalama na utulivu wa umma kote nchini.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan

Nchini Benin, mkutano huu ulipanuliwa ili kujumuisha uongozi wa jeshi, polisi, na idara ya ujasusi. Katika muhtasari wa mkutano huu usio kiwa wa kawaida wa baraza la mawaziri, serikali ilitoa maelezo ya jaribio la mapinduzi lililoshindwa.

Kulingana na serikali, uasi huo, ulioongozwa na “wavamizi,” ulianzia katika kambi ya Togbin nje kidogo ya Cotonou. Lengo la awali lilikuwa kuwateka nyara au kuwaangamiza maafisa wakuu. Kisha, walienda kwenye makazi ya rais. Huko, walitimuliwa vikali. Hapo ndipo walijieekeza kwenye makao makuu ya televisheni ya taifa—ambapo walitoa tangazo lao.

Serikali inathibitisha usaidizi wa Jeshi la Anga la Nigeria, ambalo mashambulizi yake  yaliangamiza magari ya kivita na kumrudisha nyuma adui. Serikali inabainisha kwamba ilichagua mashambulizi ya anga ili kuepuka raia kujeruhiwa; kambi ya kijeshi ambapo walikuwa wamejificha ilikuwa katika eneo la makazi. Eneo hili linahifadhi kikosi cha ECOWAS, ambacho kinaundwa na wanajeshi wa Nigeria.

Uchunguzi umeanzishwa ili kubaini wahusika na wale walioamuru shambulio hilo.

Baraza pia linaripoti uwepo wa kitengo maalum cha vikosi kutoka Côte d’Ivoire. Serikali inapongeza ushirikiano na mshikamano wa ECOWAS na hasa inazipongeza Nigeria na Côte d’Ivoire.

Maelezo yameibuka kuhusu kuachiliwa huru kwa wakuu wa jeshi la nchi kavu na wa kikosi cha walinzi wa taifa. Serikali ilithibitisha kuachiliwa huru kwa maafisa waliokamatwa na kusema kwamba tayari walikuwa wakipelekwa katika mji wa Tchaourou, kilomita 363 kaskazini mwa Cotonou, na wanajeshi waasi waliokimbia. Maafisa hao wawili walihudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri na walionekana kwenye picha. Mkuu kikosi cha walinzi wa taifa alikuwa amefungwa bandeji mkono wake wa kulia.

Hatimaye, uchunguzi umeanzishwa ili kuwabaini wahusika na wale walioamuru jaribio hilo la mapinduzi. Watawajibika kwa matendo yao, serikali ilisema. Kiongozi wa waasi anatafutwa kwa udi na uvumba na bado hajakamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *