KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ‘KITANZINI’!
Hili ni jengo la Kanisa la Ufufuo na Uzima pale Kibaha. Hasi sasa utepe bado upo na Kanisa hilo halijafunguliwa ingawa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Kiongozi wa Kanisa hilo pale Kibaha, Askofu Maximilian Machumu ametujulisha kuwa bado jengo la Kanisa hilo limewekwa utepe. Kwamba juhudi zao za kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya ili kutaka ufafanuzi kwa nini jengo la Kanisa lao bado halijafunguliwa hazikuleta tofauti yeyote.
Je, nini kimekushangaza Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 6 Desemba 2025; Saa 3:17 usiku