Kulingana na Shirika la haki za waandishi wa habari wasio na mipaka (RSF) leo Jumanne, takwimu hizi za kati ya mwanzo wa Disemba 2024 hadi mwanzo wa Disemba mwaka huu zinalinganishwa na kipindi cha miezi 12 iliyotangulia.

Eneo ambalo lilikuwa hatari zaidi kwa waandishi linasalia kuwa ni Ukanda wa Gaza ambako waandishi 29 waliuawa, ikifuatiwa na Mexico iliyokuwa na vifo 9.

Mkuu wa RSF nchini Ujerumani Anja Asterhaus amezitolea wito serikali kote ulimwenguni kuchukua hatua na kuongeza kuwa ikiwa wale wanaotoa ripoti za ukosoaji wanahofia uhuru wao ama maisha yao, ni dhahiri demokrasia iko mashakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *