
Ripoti hiyo imesema hilo litawezekana kwa kupitisha sera za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi upotevu wa bayoanuwai, uharibifu wa ardhi na uchafuzi wa mazingira.
Waandishi wa ripoti hiyo ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa: Mtazamo wa Mazingira wa Kimataifa wa miaka minne wamesema masuala hayo hayatenganishwi na yanahitaji suluhisho linalojumuisha matumizi yaliyoongezeka na motisha za kifedha ili kuachana na mafuta ya visukuku, kuhimiza mbinu endelevu za kilimo, kupunguza uchafuzi wa mazingira na taka.
Karibu wanasayansi 300 kutoka nchi 83 walichangia katika ripoti ya mwaka huu iliyotolewa kwenye Mkutano wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya.