Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. DK. Samia Suluhu Hassan, ameonyesha kusikitishwa na kifo cha mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama kilichotangazwa leo 11.12.2025 na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dk. Samia amesema;

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama. Ninatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, wananchi wa Jimbo la Peramiho, familia, ndugu, jamaa na marafiki.

“Kwa miaka 38, Mheshimiwa Mhagama amekuwa mwanachama mahiri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiongozi wa vijana, kiongozi wa wanawake, waziri katika awamu mbalimbali na mnasihi wa wengi katika siasa na maisha

“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Amina.”

Tufollow

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *