#AzamONE Unlocked π β KUFULI LIMEFUNGULIWA
Karibu kwenye ulimwengu mpya wa filamu, tamthilia na vipindi halisi vya burudani muda wote ukiwa kokote ulimwenguni.
AzamONE inazidi kukua na kuwa imara zaidi.
Habari njema ikufikie kuwa kuanzia JANUARI 2026, kutakuwa na mabadiliko ya ratiba za filamu, tamthilia na vipindi, ili kukata kiu na kuongeza ladha ya burudani kwa mtazamaji wa chaneli namba 101 kwenye kisimbuzi cha #AzamTV.
MABADILIKO YA RATIBA KWENYE TAMTHILIA
β’ SAA 3:00 USIKU hadi SAA 4:00 USIKU tamthilia zitaruka Jumatatu hadi Alhamisi.
β’ WIKIENDI – Tamthilia zitaruka IJUMAA hadi JUMAPILI
β’ Americaβs Got Talent sasa itaruka kila JUMAMOSI NA JUMAPILI SAA 12:00 JIONI.
UPANDE WA FILAMU
– #HollywoodBlockbusters zitakuwa zikiruka mapema tu SAA 1:00 USIKU kila JUMAMOSI na JUMAPILI.
Hii ndio maana halisi ya tumeifungua AzamONE. Kaa tayari kwa mwaka wenye mambo mapyaaa.
#AzamONEUnlocked