Licha ya elimu yake ya Shahada ya Uhandisi wa Kemikali na Uchakataji aliyoipata miaka 10 iliyopita kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Frednand Vyoisaka ameamua kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) mkoani Shinyanga, baada ya kukaa mtaani kwa muda mrefu akisubiri ajira bila mafanikio.
Anasema alichukua uamuzi huo baada ya kusikia kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kuwataka wahitimu wa vyuo vikuu kujiunga na mafunzo hayo ili wapate ujuzi na kujiajiri.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi