Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salama (DAWASA), kugawa maji kwa usawa kuweka ratiba ya mgao wa maji na kuhakikisha inakuwa wazi na kuzingatia usawa kwa mila mwananchi.

Waziri Aweso amesena kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam imepungua kwa zaidi ya nusu lakini yaliyopo yanapaswa kugawiwa kwa usawa bila kuweka matabaka.

Akizungumza baada ya kupiga simu wakati kikao baina ya Wahariri na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Mkama Bwire, Waziri Aweso amesema tatizo la maji Dar es Salaam limesababishwa na kutokuwapo kwa mvua za kutosha hivyo kuarthiri upatikani wa maji.

“Sasa hizi tuna ukame mvua zimechelewa kunyesha, na hili si jambo la kuficha. Niwaombe radhi wananchi wa Dar es Salaam kutokana na uoungufu huo tuwe wavumilivu Katika kipindi hiki cha mpito.”

“Nimeagiza Dawasa waitengeneze ratiba maalumu, kiwango hiki kinachopatikana sasa kigawiwe kwa usawa na kila mwananchi apate kwa uwiano sawa,”amesisitiza.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu Bwire amewaambia Wahariri kuwa uzalishaji Katika mtambo WA Ruvu Chini umeathiriia zaidi Kwa kuwa sasa unadhalisha wastani wa lita 50,000 kutoka 270,000,000 za awali Kwa siku
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *