Madereva watano wa bodaboda wamefariki dunia papo hapo baada ya kuparamiwa na lori wakiwa kijiweni eneo Makulu jijini Dodoma.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambako inadaiwa lori hilo lilikuwa linatokea kwenye barabara ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kufeli breki na kwenda kuparamia kijiwe cha Bodaboda cha Amani kilichopo kando ya barabara hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera amesema tukio hilo limetokea jana Desemba 11, 2025 saa 2:30 usiku na ambako utingo wa lori hilo alijeruhiwa.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *