Katika taarifa yake iliyotolewa leo Jumapili na msemaji wake, Katibu Mkuu ametuma rambirambi zake za dhati kwa familia za waathiriwa na kuwatakia waliojeruhiwa afuweni ya haraka.

“Tunasimama kwa mshikamano na watu na Serikali ya Australia katika wakati huu mgumu,” imesema taarifa hiyo, ikiongeza kuwa Katibu Mkuu pia anasimama na jumuiya ya Kiyahudi nchini humo na duniani kote wanapokusanyika kusherehekea sikukuu inayoashiria amani na mwanga.

Kwa mujibi wa duru za habari watu 16 wameuawa katika shambulio hilo ambalo pia limejeruhi watu wengine zaidi ya 38.

Chuki dhidi ya Wayahudi ni chuki dhidi ya ubinadamu

Bwana. Guterres amekemea bila kusita chuki dhidi ya Wayahudi katika aina zake zote, akisisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya jamii za kidini na sherehe za amani yanashambulia moja kwa moja maadili ya misingi ya uvumilivu, kuishi pamoja na utu wa binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *